KUANZISHWA KWA KANISA LA BUNDA MJINI SDA




UtanguliziJina  -  
 Bunda mjini SDA Church
Kitongoji    Posta
Kata    Bunda
Tarafa    Serengeti
Wilaya   -  Bunda
Mkoa   -   Mara 

Njozi ya kuanzishwa Kanisa hili zilianza mnamo mwaka 1998 ambapo familia zipatazo nane zilikutanika nyumbani kwa Mzee Makwasa ikiwa ni kufungua sabato na kufunga sabato.

Familia hizo ni
Gilead Mango,
James Makwasa,
Rabson Rugora ambaye sasa ni Marehemu,
Yunia Nyambega Grace Magesa,
Martha Munyaga,
Gerald Rubairo na
Emmanuel Landa.

Familia hizi zote  walikuwa washiriki wa Balili isipokuwa  Familia ya James Makwasa

Mahali walipokutanika nyumani kwa Mzee J.Makwasa.

Tunamshukuru Mungu  kwani kwa kuanzia hapo wazo la kuomba mahubiri ndipo lilipokuja
Na mzee G.Mango alipeleka ombi hilo kwa Balaza la kanisa la Balili.

Kufanyika Mahubiri
Mnamo tarehe 01/09 – 21/09/1999 chini ya Mch.Tito Rugora ambaye ndiye alikuwa mchungaji wa mtaa wa Bunda
 aliyashirikisha makanisa yote na mahubiri yakaaza katika eneo hili la kanisa.

Mch. Enock Sando  akitokea mtaa wa Ururi ndiye alikuwa mhubiri katika mahubiri hayo na watu takribani 100 walibatizwa.

Kuanza kwa kundi
Ili kutunza washiriki hao wapya Mch.T.Rugora alipendekeza  lifunguliwe kundi na Mzee Gilead Mango akachaguliwa kuwa Mkuu wa Kundi likiwa chini ya Kanisa la Balili .

Ununuzi wa jengo 
Tunamshukuru sana Mungu kwani baada ya mahubiri tulipata taarifa ya uuzwaji wa jengo ambalo ni la idara ya Elimu na Utamaduni Mali ya halmashauri ya wilaya ya Bunda Mahali ambapo tulifanyia Mahubiri
Kanisa la Balili liliwatuma wajumbe wafuatao kwenda Busegwe makao makuu ya Conference wakati huo, kuomba msaada wa fedha kwa ajili ya kununua jengo hilo lililokuwa linauzwa Milioni tatu na laki tano
Waliotumwa ni
Ndugu Mbaraka Mshitu  ambaye sasa ni marehemu
Ndugu Japhet Mkono
Ndugu Gilead Mango

Mwenyekiti wa Confeerence  Mch Migombo na Ndugu Nyarusanda aliyekuwa Mhazini wa Conference waliwapa wajumbe hao kiasi cha Tsh Milioni moja na laki tatu  (1,300,000) ikawa mwanzo wa kulipia jengo hilo .

Fedha zingine zilichangwa na washiriki wa kanisa la Balili na Kanisa la Miembeni kupitia harambee iliyoendeshwa na Mch.Karuma toka makao makuu ya Conference .

Tunapenda kumshukuru dada Shida Bitta ambaye alituunganisha na Mahuza Nyakiranganyi aliyetulipia Tsh. Laki tano (500.000) Pia Mch.T.Rugora aliyetukopesha  laki tatu (300,000).

Kupangwa kwa Kanisa
Mnamo  27/10/1999 kanisa likapangwa na kuitwa kwa jina la
Kanisa la Waadventista wa Sabato Bunda mjini
Kanisa lilianza na washiriki wapatao 160 likiongozwa na wazee watatu
                                         G.Mango 
                                         E.Bwire 
 
                                   J.Makwasa
                    N. Nyinyimbe  Mhazini wa kanisa 
                       J.Kingo    Karani wa kanisa  

Na viongozi wengine wengi waliongoza mwaka huo na mwaka uliofuata wa 2000

   Maendeleo ya Kimajengo
Ibada zilifanyika katika jengo amabalo lilikuwa halijaezekwa
Lakini ndugu yetu Mr.Masuke alituazima Turubai lake na tukawa tunafunika  ili kupata kivuli kazi iliyoongozwa na E.Landa, I.Masingija pamoja na vijana wa kanisa
Hali kadhalika bench tulizotoka nazo Balili, tulipokuwa tukimaliza ibada tulizihifadhi kwa ndugu Fini Mugaya ambaye sasa ni marehemu. 

 Kutokana na ugumu wa kazi hii ya kuweka turubai na usombaji wa bechi kila sabato
Ndugu Stephen Makumbati alitukopesha mbao za kutosha kuezeka kanisa lote
Nasi kila sabato tulimlipa Tsh. elfu tatu
Uongozi wa kanisa ulihamasisha kila mshiriki kutoa bati moja moja.

Ununuzi wa Kiwanja
Mnamo mwaka 2010 chini wa Mch.W.Malagila tulianza mchakato wa kununua kiwanja kilichokuwa kikiuzwa kinachopakana na kanisa letu Kilichokuwa mali ya Ndugu Justine Rukaka
Kiwanja hicho tulikinunua kwa thamani ya Tsh. Miolioni ishirini na tano (25,000,000) likiwemo jengo la nyumba  ambalo lilikuwa halijaezekwa
                  — Kazi tuliyoikamilisha mwaka 2011 .

Mwishoni mwa mwaka 2012 chini ya Mch.Adamu Malindi Jengo hilo tuliliezeka jengo tunalotegemea kuweka Dispesary ya Kanisa.

Kueneza injili.
Tangu kanisa hili limepangwa lineendelea kutangaza injili kwa njia mbalimbali,
 wastani wa mahubiri ya hadhara kwa mwaka ni mahubiri mawili
Wastani wa mahubiri ya nyumba kwa nyumba ni 1. kwa mwaka
 
Ongezeko la washiriki
Tumekuwa tukikuwa mwaka baada ya mwaka  kutoka washiriki 160 mpaka sasa washiriki zaidi ya 1000 Hivyo kupelekea kuzaa kundi na hatimae sasa kanisa linalofahamika kwa jina la
 Bomani SDA Church. 

Kwa sasa kanisa linalea kundi la Ellys high school kundi ambalo wengi wao ni wanafunzi tu na watumishi wachache
Kundi hili ndilo lililo liomba kanisa  letu liwalee japo kuna umbali kutoka kanisani kwetu. 

1.Kanisa limewahi kuanzisha  shule ya chekechea  chini ya Mkurugenzi wa elimu kanisani Fibi Bulenga & Mwl Haruni Kaitira  shule iliyokuwa inaendelea vizuri sana. Lakini serikali iliifunga kwa madai ya kukosa usajiri na jengo la kusomea kwani walikuwa wakisomea ndani ya jengo la kanisa
2.Kwa sababu ya kukosekana uzio kuzunguka kanisa letu wafanya biashara hufanyia biashara zao kwenye uwanja mpya wa kanisa na kuuchafua bila kufanya usafi  japo siku ya Sabato biashara haiendelei katika uwanja huo
3. Wakati kanisa linapangwa kulikuwa na vilabu vingi sana vya pombe za kienyeji kuzunguka eneo la Kanisa tunamshukuru  Mungu vilijifuta vyenyewe
Baada ya vilabu  vya pombe kujifuta, ndipo makanisa ya jumapili yalipoanza kutumia majengo hayo kwa ajili ya ibada zao nayo hatukujua yalikotokomea
4. Kutokana na kukosekana kwa uzio wa kanisa yupo mfanya biashara za CD karibu na kanisa hupiga miziki kwa sauti ya juu na kutuondolea usikivu wakati wa vipindi vya ibada zetu.

Mahusiano na jamii
Kanisa limeendelea kuwa baraka kwa jamii inayolizunguka na hatujawai kupokea malalamiko yoyote kutoka kwa jamii inayotuzunguka
Kuanzisha Dispensary ya kanisa
Kuanzisha Shule ya Kanisa
 Jengo linalokusudiwa kuwa Dispesary

Wazee wa Kanisa KUANZIA 1999 – 2014
1. Gilead Mango
2. Eliud Bwire
3. James Makwasa
4. John Masanza
5.Mgeta Ndaro
6.Nicodem Daudi
7. Joseph Juma Kingo
8. Ibrahimu Salige
9. Peter Musa
10. Joel Johnson
 
11. Zabron Marwa
12. Benas Togoi
13. Isack Masingija
14. Daniel Konna
15. Yese Robhi
16. Pharles Makongo
17. Ayubu Daniel
18. Samson Mogereja
19. Daudi Paulo
20. Benedicto Katondo 

Wajumbe walioandaa historia hii
1. Isack s.Masingija – M/kiti wa                  kikao
2. Zacharia N.Charles – Katibu wa kikao
3. Gilead Mango       -     Mjumbe
4. Benedictor Magesa  - Mjumbe
5.Grace S.Magesa        -  Mjumbe
6. Tatu Kanyonyi        -   Mjumbe
7. James Makwasa
8. Joseph Mjee
9. Edida S.Magoti
10. Stephen Makumbati
11. Clifford Rugora
12. Lenna Mango
13. Martha Munyaga
14. Felista Bwire
15. Dawson Magina
16. Dan Simbira
17. Ibrahimu Salige
18. Juma Kingo Joseph

Hisroria hii imekusanywa na Mkuu wa mawasiliano mwaka 2014

                        — Zacharia N.Charles


You may also like

No comments: